Skip to main content

TAARIFA NJEMA KWA YANGA SC

YANGA SC NEWS UPDATE










Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya taarifa kutoka Algeria kubainisha kwamba mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A dhidi ya MC Alger utachezwa palepale ulipopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na si vinginevyo.
.
Awali MC Alger kupitia rais wa klabu hiyo, Mohamed Hakim walipeleka barua CAF kuomba kubadilisha uwanja wa mechi kutoka 5 July 1962 na wakitaka kuutumia Ali la Pointe, lakini ombi lao limekataliwa. 
.
Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi, wiki hii. Uwanja wa 5 July 1962 uliopo katika Mji wa Algiers ni karibu zaidi na Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene ambao Yanga itatua leo mchana ikitokea Dar es Salaam, hivyo haitawapa wakati mgumu wa kuanzisha safari nyingine kwenda Douera unapopatikana Uwanja wa Ali la Pointe. 
.
Hata hivyo, MC Alger waliangalia mbali zaidi kwani Uwanja wa Ali la Pointe ndiyo wanautumia zaidi kwa mechi za nyumbani za ligi, hivyo wameuzoea zaidi kulinganisha na 5 July 1962. Kitendo cha CAF kutokubali ombi la wenyeji wa mchezo huo, ni hatua nzuri ambayo Yanga kwao imekuwa nafuu kwani kama mchezo huo ungepelekwa Ali la Pointe, wawakilishi hao wa Tanzania wangelazimika kufanya safari nyingine ya umbali wa kilomita 17.62 kwa gari hadi kufika Douera kutokea Algiers.

Comments

Popular posts from this blog

TETESI: Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Nyota wake 6 ambao ni Mghana Agustine Okrah, kiungo Mahlatse Skudu Makudubela

YANGA SC NEWS UPDATE #TETESI: Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Nyota wake 6 ambao ni Mghana Agustine Okrah, kiungo Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Afrika Kusini, Mkongo Joyce Lomalisa, Zawadi Mauya, Metacha Mnata na Joseph Guede kutoka nchini Ivory Coast. Taarifa za ndani zinasema tayari wa Uongozi wa Yanga SC wamemaliza kuwaongezea mikataba nyota wote watakaosalia kikosini hapo kwa msimu 2024-25 lakini majina va wachezaji hao sio sehemu ya wachezaji waliongezewa mikataba kuelekea msimu ujao wa Mashindano ndani ya Yanga SC. Yupi alistahili kubaki ndani ya Yanga msimu ujao hapo??

HAYA APA MATOKEO YOTE YA NBC PREMIER LEAGUE LEO FULL TIME

Sports and Games #NBCPL MATOKEO  Zimepigwa #hattrick mbili leo, moja ikitoka kwa Ismail Mgunda wa Ihefu na nyingine imetoka kwa …….. FT: Simba 2-0 JKT Tanzania (Saido 88’p, Onana 90’+2) FT: Geita Gold 0-2 Azam (Yeison 58’, Feisal 71’) FT: Yanga 4-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’, 79’ Musonda 52’ / Ngassa 5’) FT: Namungo 3-2 Tabora United (Buswita 19’, 28’p, Manyanya 77’ / Abbas 84’, Moses) FT: Coastal Union 0-0 KMC  FT: Mashujaa 3-0 Dodoma Jiji (Lusajo 6’, 47’, Ulomi 84’) FT: Ihefu SC 5-1 Mtibwa Sugar (Bola 5’, Chukwu 16’, Mgunda 41’, 62’, 74’ / Karihe 37’) FT: Singida FG 2-3 Kagera Sugar (Kidemile 19’, Kaseke 84’p / Mafie 40’, Mbaraka 46’, Mhilu 82” By Maximilian Damian reporter Follow us on YouTube Facebook

MTI WA SUGAR RASMI AAGA LIGI KUU NBC PREMIER LEAGUE

Sports and Games MSIMAMO: NI rasmi sasa nafasi ya nne msimu huu inamilikiwa kihalali na Coastal Union wakati vita ya kukwepa kushuka daraja moja kwa moja likisalia kwa Geita Gold na Tabora United…… Je, nani atamfuata Mtibwa Sugar???    #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #Msimamo #Standing #LeagueTable By Maximilian Damian reporter Follow us on YouTube channel Facebook