Sports and Games
Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika (CAF) wapo kwenye mchakato wa kufanya mabadiliko kidogo ya mashindano Afrika kwa sasa mashindano yatakuwa African Football League (AFL) na CAF Champion League (CCL) huku shindano la CAF Confederation Cup (CCC) likifutwa.
-Timu ambazo zitashiriki African Football League (AFL) zitakuwa timu 24 kwa kuangalia Club ranking na sio mabingwa kwenye nchi husika ila kwenye nchi husika zitaruhusiwa timu 2 tu kushiriki mashindano hata kwenye Club ranking zipo timu 4 ambazo zitaruhusiwa ni mbili tu.
-Kwa hali ilivyo vilabu vya Simba na Yanga ndio vitashiriki African Football League (AFL) bila kuangalia ushiriki wao kwenye ligi kuu ya Tanzania. Pia kombe hilo halitaathiri ushiriki wa timu kwenye mataifa yanayopeleka timu 4 kwenye mashindano ya CAF.
-Iwapo taifa lipo kwenye mataifa 12 ambayo yanapaswa kupeleka timu 4 litapeleka timu 4 iwapo kwenye club ranking unakuta taifa hilo lina timu moja tu zile zingine 3 zitashiriki klabu bingwa Afrika (CAF Champion League).
-Kuna timu zitapata bahati ya kushiriki African Football League (AFL) kama Orlando Pirates ya Afrika kusini, Wydad ya Morocco wao watashiriki African Football League bila kuangalia au kujali ushiriki wao kwenye ligi kuu ya nchini kwao hata wamalize nafasi ya 7 kwenye ligi club ranking zinawabeba.
By Maximilian Damian reporter
Follow us on
YouTube
Facebook
Comments