Skip to main content

MIGUEL GAMOND ATAJA MAFANIKIO YA YANGA

Sports and Games


#MICHEZO: Kocha wa Yanga SC Miguel Gamondi amejinasibu kuwa mafanikio waliyoyapata msimu huu ni kutokana na ubora wa wachezaji walionao. Na kikosi chake kilikuwa bora kwenye maeneo yote na ubora wao ni mkubwa ukilinganisha na wengine.

“Tulikuwa na msimu bora, tumefunga mabao mengi tumekuwa timu bora kwenye kushambulia timu bora kwenye ulinzi. Tumekuwa bora, nafikiri tumekuwa bora mbali sana kwa sababu tuna wachezaji bora, nataka niwapongeze wachezaji wote na sio Aziz peke yake.” Amesema Miguel Gamondi

Yanga imechukua ubingwa wa Ligi kuu kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Azam FC waliomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara msimu 2023-24. Yanga imemaliza ikiwa na alama 80, pia wameongoza kwa kufunga mabao 71 huku wakiruhusu mabao 14 tu ya kufungwa.


By Maximilian Damian reporter



Follow us on



YouTube





Facebook

Comments

Popular posts from this blog

Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____?

YANGA SC NEWS UPDATE Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____? Young Africans SC  𝐂𝐀𝐅𝐂𝐋 πŸπŸŽπŸπŸ’/πŸπŸ“ - π“π‡πˆπ‘πƒ πŠπˆπ“πŸ”° #TimuYaWananchi  #DaimaMbeleNyumaMwiko

TUZO ZA TFF KUTOLEWA LEO KATIKA UKUMBI WA SUPER DOME MASAKI

YANGA SC NEWS UPDATE ... 🚨 π—¨π—£π——π—”π—§π—˜π—¦ β„Ή️ Tuzo za (TFF) zitafanyika   1 Aug 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki.  Zaidi ya watu 550 watahudhulia.  β„Ή️ Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imesema kuwa, wamechelewa kutoa ratiba ya ligi kuu kwa sababu ya confirmation ya viwanja.  Bodi hiyo imeeleza kuwa, 24 | 25 wamepanga kutumia viwanja vichache ambayo ni bora ili kulinda hadhi ya ligi kuu Tanzania bara.

TAARIFA NJEMA KWA YANGA SC

YANGA SC NEWS UPDATE Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya taarifa kutoka Algeria kubainisha kwamba mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A dhidi ya MC Alger utachezwa palepale ulipopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na si vinginevyo. . Awali MC Alger kupitia rais wa klabu hiyo, Mohamed Hakim walipeleka barua CAF kuomba kubadilisha uwanja wa mechi kutoka 5 July 1962 na wakitaka kuutumia Ali la Pointe, lakini ombi lao limekataliwa.  . Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi, wiki hii. Uwanja wa 5 July 1962 uliopo katika Mji wa Algiers ni karibu zaidi na Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene ambao Yanga itatua leo mchana ikitokea Dar es Salaam, hivyo haitawapa wakati mgumu wa kuanzisha safari nyingine kwenda Douera unapopatikana Uwanja wa Ali la Pointe.  . Hata hivyo, MC Alger waliangalia mbali zaidi kwani Uwanja wa Ali la Pointe ndiyo wanautumia zaidi kwa mechi za nyumbani za ligi, hivyo wameuzoea zaidi kulinganisha na 5 July 1962. Kitendo cha CAF kutokuba...