Skip to main content

π—•π—’π—žπ—” 𝗔π—ͺπ—”π—žπ—”π—§π—”π—” π—¦π—œπ— π—•π—”

YANGA SC NEWS UPDATE


🚨 π—•π—’π—žπ—” 𝗔π—ͺπ—”π—žπ—”π—§π—”π—” π—¦π—œπ— π—•π—”

Walitaka kumuiba wing-back wa Yanga.

Mwanaspoti wamezungumza na fullback | Winga Chadrack Boka pamoja na katibu mkuu wa klabu ya FC Lupopo.

"Sikuwahi kufanya mazungumzo nao (Simba) kabla, lakini kocha wangu mmoja alinitafuta na kuniambia watu wa Simba wanakutafuta. Akawapa namba zangu wakanipigia lakini sikuwa na maongezi nao marefu"




"Niliwaambia kwamba tayari nilishasaini mkataba wa awali na Yanga SC, wakaniambia nisiende huko watajua namna ya kumaliza hilo. Nikawaambia wawatafute wenyewe Yanga au wamtafute Rais wa Yanga yeye ndiye aliyekuja huku kuongea na mimi"

©️ Chadrack Boka.

Katibu mkuu wa klabu ya FC Lupopo, Donat Mulongoy kuhusu hilo ameeleza kuwa :

"Kweli tulipokea simu za watu wa Simba SC wanasema wanajua kwamba Boka bado ni mchezaji wa FC Lupopo na wanataka kutupa pesa mara mbili ya ile Yanga wanataka kutoa kama tukikubali kufanya biashara"




"Tumewaambia hakuna namna mambo yanaweza kubadilika kwa kuwa kila kitu kimemalizika muda mrefu, kama wao bado wanamtaka mchezaji wasubiri afike Tanzania wataongea na watu wa Yanga"

"Lupopo hatuzuii kufanya biashara, zipo timu ambazo hatuwezi kufanya nazo biashara hata za mchezaji mmoja na hizo timu zipo hapa Congo, lakini nje ya hapa tunaweza kufanya biashara na timu yoyote"

"Kwa hili la Boka hakuna njia tunaweza kupindua mambo kwa kuwa kila kitu kimemalizika vizuri. Yanga walikuja hapa tukaongea na Rais wao na baadae Rais wetu Bwana Kyabula Jacques amekuja Tanzania, wakatuma tena mtu hapa tukamaliza hiyo biashara. Kitu kilichobakia ni Yanga kumlketa mchezaji huko Tanzania kwa muda watakaoona unafaa"


Comments

Popular posts from this blog

Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____?

YANGA SC NEWS UPDATE Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____? Young Africans SC  𝐂𝐀𝐅𝐂𝐋 πŸπŸŽπŸπŸ’/πŸπŸ“ - π“π‡πˆπ‘πƒ πŠπˆπ“πŸ”° #TimuYaWananchi  #DaimaMbeleNyumaMwiko

TUZO ZA TFF KUTOLEWA LEO KATIKA UKUMBI WA SUPER DOME MASAKI

YANGA SC NEWS UPDATE ... 🚨 π—¨π—£π——π—”π—§π—˜π—¦ ℹ️ Tuzo za (TFF) zitafanyika   1 Aug 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki.  Zaidi ya watu 550 watahudhulia.  ℹ️ Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imesema kuwa, wamechelewa kutoa ratiba ya ligi kuu kwa sababu ya confirmation ya viwanja.  Bodi hiyo imeeleza kuwa, 24 | 25 wamepanga kutumia viwanja vichache ambayo ni bora ili kulinda hadhi ya ligi kuu Tanzania bara.

TAARIFA NJEMA KWA YANGA SC

YANGA SC NEWS UPDATE Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya taarifa kutoka Algeria kubainisha kwamba mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A dhidi ya MC Alger utachezwa palepale ulipopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na si vinginevyo. . Awali MC Alger kupitia rais wa klabu hiyo, Mohamed Hakim walipeleka barua CAF kuomba kubadilisha uwanja wa mechi kutoka 5 July 1962 na wakitaka kuutumia Ali la Pointe, lakini ombi lao limekataliwa.  . Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi, wiki hii. Uwanja wa 5 July 1962 uliopo katika Mji wa Algiers ni karibu zaidi na Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene ambao Yanga itatua leo mchana ikitokea Dar es Salaam, hivyo haitawapa wakati mgumu wa kuanzisha safari nyingine kwenda Douera unapopatikana Uwanja wa Ali la Pointe.  . Hata hivyo, MC Alger waliangalia mbali zaidi kwani Uwanja wa Ali la Pointe ndiyo wanautumia zaidi kwa mechi za nyumbani za ligi, hivyo wameuzoea zaidi kulinganisha na 5 July 1962. Kitendo cha CAF kutokuba...