(FIFA), (CAF) na mashirikisho mengine yote yana mitandao ya kijamii, lakini hayajawahi kuposti wadaiwa au maamuzi dhidi ya wadaiwa wao, hizi huwa
YANGA SC NEWS UPDATE
ANAANDIKA MWANASHERIA WA KLABU YA YANGA SC
"(FIFA), (CAF) na mashirikisho mengine yote yana mitandao ya kijamii, lakini hayajawahi kuposti wadaiwa au maamuzi dhidi ya wadaiwa wao, hizi huwa internal communication (mawasiliano ya ndani).
Suala la kudaiwa na wachezaji ni suala la kawaida kwenye soka
Mpaka leo hii vilabu vikubwa kama TP Mazembe, Raja Club Athletic, Wydad, Zamalek, Belouzdad, Club Africain zote bado zimefungiwa ila FIFA, CAF wala Mashirikisho yao hawajawapost kwenye mitandao ya kijamii, unajua kwanini?
Kama ni habari za kupost zipo nyingi na zenye manufaa kwa jamii yetu, mfano Rais Karia jana alikua Tabora kwenye majukumu ya kulipambania soka la Tanzania ametoa habari njema kwa wana Tabora, nilitarajia kuiona."
Na nyie ndugu zangu wananchi, kama hizi taarifa zinawakwaza, dawa ni moja tu, kulipa ada, kwani dawa ya deni ni kulipa hakuna miujiza mingine, katika kujenga Yanga muitakayo wachezaji watakuja na kuondoka na hakuna mfadhili atakuja kulipa madeni, tuisapoti Transformation kwa vitendo.
Haya ni maoni yangu binafsi kama shabiki wa mpira!
NB : Nawakumbusha tu, Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi za watu na taasisi imeshaanza kufanya kazi, isomeni mtanishukuru badae." - Simon Patrick, Mwanasheria wa klabu Yanga SC.
Comments