Skip to main content

HATMA YA GUEDE KUJULIKANA SIKU YA J TATU

YANGA SC NEWS UPDATES


MBIVU NA MBICHI GUEDE KUJULIKANA JUMATATU



Klabu ya Yanga inatarajiwa kutoa taarifa juu ya hatima ya mshambuliaji Joseph Guede ambaye mkataba wake umemalizika

Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa Guede alisaimi mkataba wa miezi sita na sasa mkataba wake umemalizika

Siku chache zilizopita kumeibuka tetezi kuwa Yanga inamuwania mshambuliaji wa Al Nasri ya Libya na timu ya Taifa ya Ghana Jonathan Sowah ambaye amewahi kuitumikia Medeama Fc iloyokuwa kundi moja na Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita

Sowah anatajwa kutua Yanga kuchukua nafasi ya Guede, Kamwe amesema Hatma ya mshambuliaji huyo itafahamika Jumatatu

"Suala la Guede ni tofauti kidogo yeye mkataba wake umemalizika kwani alisaini mkataba wa miezi sita wakati tulipomsajili January. Kumekuwa na majadiliano kuhusu kumuongezea mkataba hivyo taarifa yake na nyingine zote za usajili tutaanza kuzitoa siku ya Jumatatu,"alisema Kamwe

Kumekuwa na taarifa kuwa mchakato wa kumuongezea Guede mkataba ulikwama baada ya kutofikia makubaliano ya pande zote mbili

Inaelezwa Guede amepata ofa nono zaidi na huenda akaelekea Uarabuni


Sisi ndo yanga usiache kufuatilia tovuti yetu ya yanga sc news kupitiaπŸ‘‡πŸ‘‡

Ili uweze kupata habari zetu za yanga SC kila siku!!

Comments

Popular posts from this blog

Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____?

YANGA SC NEWS UPDATE Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____? Young Africans SC  𝐂𝐀𝐅𝐂𝐋 πŸπŸŽπŸπŸ’/πŸπŸ“ - π“π‡πˆπ‘πƒ πŠπˆπ“πŸ”° #TimuYaWananchi  #DaimaMbeleNyumaMwiko

TUZO ZA TFF KUTOLEWA LEO KATIKA UKUMBI WA SUPER DOME MASAKI

YANGA SC NEWS UPDATE ... 🚨 π—¨π—£π——π—”π—§π—˜π—¦ β„Ή️ Tuzo za (TFF) zitafanyika   1 Aug 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki.  Zaidi ya watu 550 watahudhulia.  β„Ή️ Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imesema kuwa, wamechelewa kutoa ratiba ya ligi kuu kwa sababu ya confirmation ya viwanja.  Bodi hiyo imeeleza kuwa, 24 | 25 wamepanga kutumia viwanja vichache ambayo ni bora ili kulinda hadhi ya ligi kuu Tanzania bara.

TAARIFA NJEMA KWA YANGA SC

YANGA SC NEWS UPDATE Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya taarifa kutoka Algeria kubainisha kwamba mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A dhidi ya MC Alger utachezwa palepale ulipopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na si vinginevyo. . Awali MC Alger kupitia rais wa klabu hiyo, Mohamed Hakim walipeleka barua CAF kuomba kubadilisha uwanja wa mechi kutoka 5 July 1962 na wakitaka kuutumia Ali la Pointe, lakini ombi lao limekataliwa.  . Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi, wiki hii. Uwanja wa 5 July 1962 uliopo katika Mji wa Algiers ni karibu zaidi na Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene ambao Yanga itatua leo mchana ikitokea Dar es Salaam, hivyo haitawapa wakati mgumu wa kuanzisha safari nyingine kwenda Douera unapopatikana Uwanja wa Ali la Pointe.  . Hata hivyo, MC Alger waliangalia mbali zaidi kwani Uwanja wa Ali la Pointe ndiyo wanautumia zaidi kwa mechi za nyumbani za ligi, hivyo wameuzoea zaidi kulinganisha na 5 July 1962. Kitendo cha CAF kutokuba...