Skip to main content

YANGA NI HATARI WANAPOKUWA HAWANA MPIRA : RANGA CHIVAVILO MSHAMBULIAJI KAIZER CHIEFS

YANGA SC NEWS UPDATE


YANGA NI HATARI WANAPOKUWA HAWANA MPIRA : RANGA CHIVAVILO MSHAMBULIAJI KAIZER CHIEFS 

Mshambuliaji wa Kaizer Chiefs Ranga Chivaviro amekiri kuwa ubora wa Yanga ikiwa haina mpira ndio imewapa ushindi wa mabao 4-0 wa Toyota Cup uliopigwa Afrika Kusini Jumapili iliyopita 

Katika mchezo huo Prince Dube, Aziz Ki na Clement Mzize ndio waliofunga mabao ya Yanga huku mawili yakifungwa na Aziz Ki

Ki alifunga mabao hayo yakiwa ni matokeo ya 'pressing' iliyofanywa na wachezaji wa Yanga na kupelekea walinzi wa Kaizer Chiefs kufanya makosa 

Chivaviro alianza katika mchezo huo akiongoza safu ya ushambuliaji ya Chiefs lakini mpaka kocha Nasreddine Nabi anamtoa hakuwa amepiga shuti lolote langoni kwa Yanga

"Ilikuwa ngumu kwetu, ni kama hawakutupa nafasi ya kujipanga wakati tukiwa tuna mpira, walikuwa wanalazimisha haraka tuupoteze uwe chini yao nadhani ndio silaha walioitumia kutengeneza ushindi wao"

"Unajua huu ulikuwa mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki wenzetu walionekana kuwa wepesi kuliko sisi ilitufanya tuonekane hatukuwa tayari kukutana nao, nadhani tutabadilika kwakuwa tuko chini ya makocha wapya ambao wanaanza kutupa falsafa mpya," alisema Chivaviro

Yanga ilibeba taji la Toyota Cup baada ya ushindi huo huku Wananchi pia wakikomba zaidi ya shilingi milioni 260 


Comments

Popular posts from this blog

Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____?

YANGA SC NEWS UPDATE Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____? Young Africans SC  𝐂𝐀𝐅𝐂𝐋 πŸπŸŽπŸπŸ’/πŸπŸ“ - π“π‡πˆπ‘πƒ πŠπˆπ“πŸ”° #TimuYaWananchi  #DaimaMbeleNyumaMwiko

TUZO ZA TFF KUTOLEWA LEO KATIKA UKUMBI WA SUPER DOME MASAKI

YANGA SC NEWS UPDATE ... 🚨 π—¨π—£π——π—”π—§π—˜π—¦ ℹ️ Tuzo za (TFF) zitafanyika   1 Aug 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki.  Zaidi ya watu 550 watahudhulia.  ℹ️ Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imesema kuwa, wamechelewa kutoa ratiba ya ligi kuu kwa sababu ya confirmation ya viwanja.  Bodi hiyo imeeleza kuwa, 24 | 25 wamepanga kutumia viwanja vichache ambayo ni bora ili kulinda hadhi ya ligi kuu Tanzania bara.

TAARIFA NJEMA KWA YANGA SC

YANGA SC NEWS UPDATE Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya taarifa kutoka Algeria kubainisha kwamba mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A dhidi ya MC Alger utachezwa palepale ulipopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na si vinginevyo. . Awali MC Alger kupitia rais wa klabu hiyo, Mohamed Hakim walipeleka barua CAF kuomba kubadilisha uwanja wa mechi kutoka 5 July 1962 na wakitaka kuutumia Ali la Pointe, lakini ombi lao limekataliwa.  . Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi, wiki hii. Uwanja wa 5 July 1962 uliopo katika Mji wa Algiers ni karibu zaidi na Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene ambao Yanga itatua leo mchana ikitokea Dar es Salaam, hivyo haitawapa wakati mgumu wa kuanzisha safari nyingine kwenda Douera unapopatikana Uwanja wa Ali la Pointe.  . Hata hivyo, MC Alger waliangalia mbali zaidi kwani Uwanja wa Ali la Pointe ndiyo wanautumia zaidi kwa mechi za nyumbani za ligi, hivyo wameuzoea zaidi kulinganisha na 5 July 1962. Kitendo cha CAF kutokuba...