Skip to main content

π™†π˜Όπ™ˆπ™’π™€ π˜Όπ™†π™€π™π™’π˜Ό π™”π˜Όπ™‰π™‚π˜Ό π™†π™π™π™π™ˆπ™„π™†π˜Ό π™‰π˜Ό π™ˆπ˜Όπ™’π˜Όπ™†π˜Όπ™‡π˜Ό

YANGA SC NEWS UPDATE


π™†π˜Όπ™ˆπ™’π™€ π˜Όπ™†π™€π™π™’π˜Ό π™”π˜Όπ™‰π™‚π˜Ό π™†π™π™π™π™ˆπ™„π™†π˜Ό π™‰π˜Ό π™ˆπ˜Όπ™’π˜Όπ™†π˜Όπ™‡π˜Ό


Meneja wa idara ya habari na mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kuwa baadhi ya mawakala wanaitumia klabu hiyo kwa ajili ya kuwapa thamani wachezaji wao na kuwauza kwa dau kubwa.




 Kamwe amesema baadhi ya mawakala wa wachezaji wamekuwa na tabia ya kuwahusisha wachezaji kuwa wanatakiwa na Yanga ili kuzifanya timu zingine zipande dau wakati si kweli kama wanawahitaji.

Kamwe alisema vitendo hivyo vilifanyika msimu uliopita na anashangaa msimu huu vimeibuka tena, akiwataka mawakala kuwauza wachezaji kwa thamani zao halisi na kuacha kuitumia Yanga kwa njia ya kuwapandisha thamani na kupata pesa nyingi za usajili.

"Mwaka jana hawa mawakala walitengeneza stori kuwa kuna mchezaji Yanga inamtaka, lakini alipokwenda klabu nyingine ikasemekana eti ameibiwa Uwanja wa Ndege, sisi wala hatukusema kitu," alisema Kamwe.





Ingawa hakufafanua, lakini ukirejea moja ya stori za matukio ya msimu uliopita ilisemekana kuwa Simba ilimpora mchezaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Fabrice Ngoma, Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, akiwa anakuja kusaini mkataba Klabu ya Yanga.

"Kuelekea msimu unaokuja tunaanza kusikia tena habari kama zile, wanasema kuna kiungo tumepokonywa, si kweli ukiona hivyo hatukumhitaji, hivyo ni kazi ya mawakala kupiganisha ili wapige pesa," alisema Ofisa Habari huyo.

Hivi karibuni katika tetesi za usajili inadaiwa ilikuwa katika hatua za mwisho kumsajili kiungo mkabaji wa Singida Black Stars, Yusuph Kagoma, lakini taarifa zilizokuja baadaye zikaeleza, Simba imepindua meza na kumsainisha mkataba wa miaka mwili.

Hata hivyo, bado Simba haijathibitisha rasmi kumsajili mchezaji huyo mpaka sasa.

Akizungumzia usajili, Kamwe alisema tayari wameshamaliza kazi iliyobaki ni kuwatangaza tu.

Tangu awali, Yanga ilitangaza kuwa haitofanya usajili mkubwa sana kwani bado ina kikosi imara, na ilichofanya ni kuzuia wachezaji wake muhimu kubaki, na kufanya usajili wa wachezaji wachache tu wenye viwango vya hali ya juu kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi.

"Malengo tuliyonayo ni makubwa na usajili tulioufanya, watu watalia na kusaga meno," alisema Kamwe.

Tetesi zinadai kuwa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji, Emmanuel Bola Lobota, winga kutoka Singida Black Stars, Agee Basiala, kiungo mshambuliaji kutoka AS Maniema Union na beki wa kushoto, Chadrack Boka kutoka Klabu ya Saint Eloi Lupopo, wote hao kutoka DR Congo.

Mwingine ni kipa Khomein Abubakar wa Singida Black Stars, anayekwenda kuchukua nafasi ya Metacha Mnata, anayetajwa kuondoka msimu ujao.








KAMA UNATUMIA MTANDAO WA TIGO!!! HII NIKWAAJILI YAKO!!!

Nenda kwenye Google play store

Download app ya Tigo pesa then jisajili kisha Nenda sehem ilioandikwa *Invite& Earn* Gusa pale then gusa neno "REDEEM" au KOMBOA afu kwenye Code jaza "TBN6439Y" Tayali apo utapata Gb 1 na shiling 2000 Kutoka tigo

KUMBUKA KUJAZA HILI NENO HAPO CHINI
            πŸ‘‡πŸ‘‡

          TBN6439Y




Comments

Popular posts from this blog

TETESI: Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Nyota wake 6 ambao ni Mghana Agustine Okrah, kiungo Mahlatse Skudu Makudubela

YANGA SC NEWS UPDATE #TETESI: Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Nyota wake 6 ambao ni Mghana Agustine Okrah, kiungo Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Afrika Kusini, Mkongo Joyce Lomalisa, Zawadi Mauya, Metacha Mnata na Joseph Guede kutoka nchini Ivory Coast. Taarifa za ndani zinasema tayari wa Uongozi wa Yanga SC wamemaliza kuwaongezea mikataba nyota wote watakaosalia kikosini hapo kwa msimu 2024-25 lakini majina va wachezaji hao sio sehemu ya wachezaji waliongezewa mikataba kuelekea msimu ujao wa Mashindano ndani ya Yanga SC. Yupi alistahili kubaki ndani ya Yanga msimu ujao hapo??

HAYA APA MATOKEO YOTE YA NBC PREMIER LEAGUE LEO FULL TIME

Sports and Games #NBCPL MATOKEO  Zimepigwa #hattrick mbili leo, moja ikitoka kwa Ismail Mgunda wa Ihefu na nyingine imetoka kwa …….. FT: Simba 2-0 JKT Tanzania (Saido 88’p, Onana 90’+2) FT: Geita Gold 0-2 Azam (Yeison 58’, Feisal 71’) FT: Yanga 4-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’, 79’ Musonda 52’ / Ngassa 5’) FT: Namungo 3-2 Tabora United (Buswita 19’, 28’p, Manyanya 77’ / Abbas 84’, Moses) FT: Coastal Union 0-0 KMC  FT: Mashujaa 3-0 Dodoma Jiji (Lusajo 6’, 47’, Ulomi 84’) FT: Ihefu SC 5-1 Mtibwa Sugar (Bola 5’, Chukwu 16’, Mgunda 41’, 62’, 74’ / Karihe 37’) FT: Singida FG 2-3 Kagera Sugar (Kidemile 19’, Kaseke 84’p / Mafie 40’, Mbaraka 46’, Mhilu 82” By Maximilian Damian reporter Follow us on YouTube Facebook

MTI WA SUGAR RASMI AAGA LIGI KUU NBC PREMIER LEAGUE

Sports and Games MSIMAMO: NI rasmi sasa nafasi ya nne msimu huu inamilikiwa kihalali na Coastal Union wakati vita ya kukwepa kushuka daraja moja kwa moja likisalia kwa Geita Gold na Tabora United…… Je, nani atamfuata Mtibwa Sugar???    #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #Msimamo #Standing #LeagueTable By Maximilian Damian reporter Follow us on YouTube channel Facebook