Kiungo wa Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki amekata mzizi wa fitina juu ya mustakabali wake kufuatia taharuki
Sports and Games
Kiungo wa Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki amekata mzizi wa fitina juu ya mustakabali wake kufuatia taharuki iliyozuka miongoni mwa wapenzi wa soka baada ya posti yake aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii kuzua sintofahamu.
Awali kiungo huyo raia wa Burkina Faso alichapisha taarifa ya kuushukuru uongozi wa klabu hiyo, mashabiki pamoja za wachezaji wenzie kwa mafanikio waliyoyapata katika msimu uliomalizika hali iliyopelekea wengi kudhani anaaga Yanga.
Hata hivyo Aziz Ki amejibu 'comment' ya mdau iliyosema βAshiiii Azizi sasa kwenye post yako usianze na maneno 'thanks' unatufanye tuhofie kuwa unataka kuondokaβ
Akijibu 'comment' hiyo Ki ameandika βNawashukuru kwa sababu ni jambo dogo sana ninaloweza kufanya kuwashukuru nyinyi ambao mnanisaidia kila siku, SIO KWAHERI NIKO HAPA MSIJALIβ
Posti iliyozua sintofahamu ilisomeka "Kila kitu kiliwezekana Shukrani kwenu wachezaji wenzangu, wafanyakazi, kamati ya rais na hasa nyinyi mashabiki, wapendwa wangu, familia na pia kwa baraka za Mungu mwema
kwa mara nyingine tena asante kwa uaminifu wako, msaada wako, imani yako, umenipa mengi katika msimu wote
BY Maximilian Damian reporter.
Follow us on
Facebook
KARIBU UTANGAZE NASI BIASHARA YAKO WASILIANA NASI KUPITIA WHATSAPP BOFYA HAPA
ππ
AU TUPIGIE KUPITIA+2556941267
OR
+255653393434
Comments