Skip to main content

Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Mtoto Albino, Asimwe Novart ambaye alichukuliwa nyumbani

YANGA SC NEWS UPDATE



Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Mtoto Albino, Asimwe Novart ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu Mkoani Kagera May 30, 2024 na mwili wake kukutwa kwenye kalavati, June 17,2024 akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao.

Mkuu wa mashtaka Mkoa wa Kagera Waziri Mangumbo akisaidiana na Wakili wa Serikali, Erick Mabagala wamewasomea mashtaka yao Watuhumiwa hao tisa kuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya makusudi huku akisema kuwa uchunguzi wa shauri hilo no 17740 la mwaka 2024 tayari umekamilika.

Shitaka hilo limesomwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Elipokea Yona Wilson ambaye amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na wamerudishwa rumande mpaka July 12,2024 ambapo kesi yao itatajwa tena.

Watuhumiwa hao tisa ni Elpidius Alfred Rwegoshora (49) ambaye ni Padri, Novat Venant (24) ambaye ni Baba wa Mtoto, Nurdin Ahmada, Ramadhan Selestine,Rwenyagira Alphonce, Dastan Buchard, Faswiu Athuman,Gozibert Arikad na Dezdery Everigist. 

Comments

Popular posts from this blog

Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____?

YANGA SC NEWS UPDATE Klabu ya Yanga SC imefanya uzinduzi wa jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/25 Unazipa Marks ngapi kati ya 10____? Young Africans SC  𝐂𝐀𝐅𝐂𝐋 πŸπŸŽπŸπŸ’/πŸπŸ“ - π“π‡πˆπ‘πƒ πŠπˆπ“πŸ”° #TimuYaWananchi  #DaimaMbeleNyumaMwiko

TUZO ZA TFF KUTOLEWA LEO KATIKA UKUMBI WA SUPER DOME MASAKI

YANGA SC NEWS UPDATE ... 🚨 π—¨π—£π——π—”π—§π—˜π—¦ ℹ️ Tuzo za (TFF) zitafanyika   1 Aug 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki.  Zaidi ya watu 550 watahudhulia.  ℹ️ Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imesema kuwa, wamechelewa kutoa ratiba ya ligi kuu kwa sababu ya confirmation ya viwanja.  Bodi hiyo imeeleza kuwa, 24 | 25 wamepanga kutumia viwanja vichache ambayo ni bora ili kulinda hadhi ya ligi kuu Tanzania bara.

TAARIFA NJEMA KWA YANGA SC

YANGA SC NEWS UPDATE Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga baada ya taarifa kutoka Algeria kubainisha kwamba mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A dhidi ya MC Alger utachezwa palepale ulipopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na si vinginevyo. . Awali MC Alger kupitia rais wa klabu hiyo, Mohamed Hakim walipeleka barua CAF kuomba kubadilisha uwanja wa mechi kutoka 5 July 1962 na wakitaka kuutumia Ali la Pointe, lakini ombi lao limekataliwa.  . Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi, wiki hii. Uwanja wa 5 July 1962 uliopo katika Mji wa Algiers ni karibu zaidi na Uwanja wa Ndege wa Houari Boumediene ambao Yanga itatua leo mchana ikitokea Dar es Salaam, hivyo haitawapa wakati mgumu wa kuanzisha safari nyingine kwenda Douera unapopatikana Uwanja wa Ali la Pointe.  . Hata hivyo, MC Alger waliangalia mbali zaidi kwani Uwanja wa Ali la Pointe ndiyo wanautumia zaidi kwa mechi za nyumbani za ligi, hivyo wameuzoea zaidi kulinganisha na 5 July 1962. Kitendo cha CAF kutokuba...